LISTEN LIVE

    

REDIO MAARIFA NI MOJA KATIKA REDIO KUBWA KATIKA UKANDA WA TANZANIA.

Kufuatia Kuanzishwa Kwa Urushwaji wa Masafa ya Kielectronic ya Habari Tanzania,REDIO MAARIFA Ikiwa na Studio zake Jijini Tanga,Tanzania Imejiridhisha na Kufanikiwa kuwa na Vijana na Nguvu Kazi endelevu yenye kutenda Kazi Kwa Ufanisi. Watendaji na watumishi wake wameweza kuwa na Uzoefu katika kurusha Matangazo na Ufanisi Mkubwa katika Uzalishaji wa Vipindi.

Kituo kinarusha Matangazo yake masaa 24 lengo ni Kuweza kumridhisha Msikilizaji wetu na Kuweza kuendelea kuwepo katika soko kupitia urushaji wa Vipindi vyenye ubora wa hali ya Juu.

Kituo kina Idara Nne, ambazo ni Idara ya Tafiti, Idara ya Mauzo na Masoko, Idara ya Habari na Watangazaji, Idara ya Uzalishaji.

Pia tumeendelea kutoa Mafunzo mbalimbali Kwa wanahabari katika Asasi Kubwa za Habari ikiwa ni katika sehemu yetu tuliodhamiria katika lengo la Jamii tunayoihabarisha Habari mbalimbali.

Tumeamua kutoa Vipindi vyetu Kwa matakwa ya Msikilizaji wetu. Tumeweza kutoa Vipeperushi Katika Maeneo mbalimbali ya Nchi Pamoja na kupokea maoni mbalimbali kupitia Mitandao ya Kijamii inayohusisha Simu, Ujumbe, WhatsApp na pia kutembelewa katika Studio Zetu,Jumbe za Vipeperushi hivi pia vimekuwa vikirushwa katika Kituo chetu Cha REDIO na Mapokeo yake yamekua ni Makubwa.Na Baada ya Kufanyia Utafiti Maoni ya wasikilizaji wetu, Wataalamu wetu Waliobobea katika tasnia ya Habari,wamekaa Chini na Kuweza Kufanyia Kazi mapendekezo ya wasikilizaji wetu. Pamoja na kuwa Vipindi Vyetu Vimekua vya Kipekee sana Bali vimeweza kushangaza na Kuvutia Vyombo vingine vya Habari kutokana na utendaji kazi wetu.

Wasilia Nasi:
admin@maarifaradio.co.tz
+255 767 957383 | +255 710 288508